Toshiba yapata oda la kuunda mfumo wa kuzalisha kawi kutokana na nishati ya mvuke kwa kiwango cha chini nchini Ethiopia kwa kutumia teknolojia ya kisasa

Toshiba yapata oda la kuunda mfumo wa kuzalisha kawi kutokana na nishati ya mvuke kwa kiwango cha chini nchini Ethiopia kwa kutumia teknolojia ya kisasa

KAWASAKI, Japan, 28 Februari 2020, -/African Mdia Agency (AMA)/- Toshiba Energy Systems & Solutions Corporation (kwa ufupisho “Toshiba ESS”) leo imetangaza ya kwamba kampuni hiyo, Toyota Tsusho Corporation na kampuni ya uhandisi ya Uturuki-Egesim Energy Electro-Mechanic Construction Contracting Co., Ltd. imepata oda ya uhandisi, uagizaji na ujenzi wa mfumo wa kuzalisha kawi inayotokana na nishati ya mvuke kwa kutumia teknolojia ya kisasa (Wellhead) eneo la Aluto Langano iliyopo katikati mwa Ethiopia chini ya usimamizi wa Kampuni ya Umeme ya Ethiopia (kwa ufupisho “EEP”).

Kampuni ya Toshiba ESS itakuwa na jukumu la kusambaza mitambo ya kutengeneza kawi kutokana na mvuke na pia jenereta.
Mradi huu utaendelea kupitia kwa mpango wa utoaji msaada kutoka kwa serikali ya Japan kupitia kwa shirika la Japan International Cooperation Agency (JICA).
Mradi wa nishati ya mvuke wa Aluto Langano utakuwa ni kiwanda cha uzalishaji kawi kwa kiwango cha chini cha megawati tano (5), ambamo EEP inapanga kuzindua operesheni za kibiashara Agosti 2021.

Toshiba ESS itaunda mfumo wa kuzalisha kawi kwa kiwango cha chini ndani ya kiwanda hiki. Mfumo huo wa kuzalisha umeme unaotokana na nishati ya mvuke, ambao umeundwa na Toshiba ESS utakuwa na uwezo wa kutoa kawi ya kati ya megawati moja hadi megawati ishirini. Unaweza kufungwa kwa muda mfupi ili kuanza operesheni haraka. Ni mfumo wa kuzalisha nguvu za umeme unaoweza kubebwa na unaoweza kutumia idadi ndogo ya visima vilivyochimbwa.

Ethiopia ni taifa la pili kuwa na watu wengi zaidi Afrika kwa kuwa na watu zaidi ya milioni mia moja. Ingawa taifa hilo linaendelea kukua kiuchumi, kiwango cha usambazaji wa umeme kimesalia kuwa asilimia thelathini pekee (30*). Hivyo, taifa hilo linakabiliwa na haja ya kuongeza viwanda vya kuzalisha kawi.

Ethiopia ina uwezo wa kuzalisha megawati elfu kumi (10,000 *) kutokana na uwezo mkubwa wa nishati ya mvuke na inapanga kujenga viwanda vipya vya kuzalisha kawi kutokana na nishati hiyo vyenye uwezo wa kutoa megawati takriban elfu mbili mia tano (2,500) za umeme kufikia mwaka wa elfu mbili na thelathini(2030).
Toyoaki Fujita, msimamizi wa maendeleo ya biashara wa Toshiba ESS, alisema, “Tumefurahi sana kupokea oda hiyo ya kutengeneza mfumo wa kawi ambao ni mradi wetu wa kwanza wa umeme nchini Ethiopia.

Tulitia sahihi hati ya maelewano (MOU) ya uhusiano wa kina na EEP katika uzalishaji wa nishati ya mvuke Septemba 2014. Kwa kuzingatia maelewano hayo, tumekuwa tukiwasaidia katika kukuza utaalam kama vile kutoa mafunzo kwa maafisa na wasimamizi wake katika kampuni yetu kwa kutumia mipango kadhaa ya utoaji msaada na serikali. Waziri Mkuu wa Ethiopia alipozuru Japan Agosti mwaka wa elfu mbili kumi na tisa (2019), alitembelea kituo chetu cha Keihin Product Operations kuona teknolojia yetu ya kutengeneza umeme kutokana na nishati ya mvuke.
Kuendelea mbele, tutadumisha miradi inayoendelea katika ukuzaji wa taaluma na kuchangia katika ukuzaji wa uzalishaji wa kawi kutokana na nishati ya mvuke nchini Ethiopia.”

Habari imesambazwa na African Media Agency (AMA) kwa niaba ya Toshiba

Ziada: Mkutano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Ethiopia na Japan (Agosti, 2019), ulioendeshwa na Wizara ya Maji, Unyunyiziaji and Kawi, Demokrasia ya Ethiopia.

Muhtasari wa Mradi
Jina la Mradi: Mfumo wa nishati ya mvuke wa Aluto Langano kwa kutumia teknolojia ya kisasa
Mmiliki: Kampuni ya Kawi ya Ethiopia (Ethiopian Electric Power- EEP)
Mwanakandarasi: Toyota Tsusho Corporation
Eneo: Aluto Langano, eneo la Shewa Mashariki, eneo kubwa la Oromia, Ethiopia
Toshiba ESS kusambaza: Mfumo mmoja wa mtambo wa kuzalisha kawi kutokana na nguvu za mvuke kwa kuzalisha umeme kwa kiwango kidogo cha megawati tano.
Siku iliyopangwa ya kuanza operesheni za kibiashara: Agosti 2021

Kwa maelezo zaidi, Tafadhali wasiliana na:
Japhet Kirimi
Media & Content Director
Engage burson cohn & wolfe
[email protected]
M: +254.763.995.487 | T: @japhetkarimi

Source link